Dondoo
Ili uweze kujisajili utahitajika kujaza majina yako, mawasiliano yako, idara, mahali ulipo na mahali unapohitaji kuhamia (mkoa na wilaya).
Mahali (Mikoa na Wilaya)
Ikiwa una chaguo zaidi ya moja juu ya wapi unahitaji kuamia, usijali, jisajili kwa mkoa na wilaya moja na baada ya kukamilisha usajili tembelea ukurasa wa mpangilio ambapo pana kitufe cha 'Hariri Mpangilio' (upande wa kushoto). Bofya kitufe hicho, kisha jaza fomu ya kuhariri mahitaji yako. Hapo unaweza kuongeza mkoa na/au wilaya mbili (kama ukihitaji) na kufanya uwe na jumla ya chaguzi tatu.
Dondoo
Kwa kawaida kila unapoingia kwenye account yako, mfumo utakuletea orodha ya walimu ikianzia na wanolingana na mahitaji (yaani wanaotaka kuondoka unapotaka kwenda, na wanaotaka kuja unapotaka kuondoka) yako bila hata ya kutafuta mwenyewe.
Zingatia:
Ili uweze kuwasiliana na mwalimu anayehitaji kubadilishana kituo cha kazi na wewe, nambari yako ya simu itawekwa wazi. Jaribu kuwa makini na simu utazopokea maana kuna uwezekano wa walimu wengine kutokuwa waaminifu au kuwa walimu hewa...!
Hamafasta ni mfumo unaokutanisha watumishi wenye uhitaji wa kuhama kutoka kituo kimoja cha kazi kwenda kituo kingine. Mfumo huu ulianza rasmi mwezi mei mwaka 2016 chini ya mwasisi mhandisi NOMBO, Ignas A.